Mkuu wa Jeshi la polisi nchini, IGP Simon Sirro, ametilia mashaka mifumo ya umeme na umathubuti wa jengo la bweni la shule ya msingi Byamungu lililowaka moto na kusababisha vifo vya watoto 10.

Sambamba na mashaka hayo, IGP Sirro amesema wanaendelea na uchunguzi wa kina ili kutambua kama kuna chanzo kingine kilichosababisha moto huo huku jeshi la polisi likiwa limemkamata mwenye shule.

“Na tukipata taarifa kamili niwahakikishie waandishi wa habari tutawashugulikia kwelikweli, hatuna mchezo na mtu ambae kwa uzembe wake au kwa nia yake hovyo anasababisha vifo vya watu, niliwahi kusema damu ya mtanzania huwa haiendi hovyo,” amesema IGP Sirro.

Aidha ameagiza kutafutwa kwa Afisa Elimu na wakaguzi wote waliokuwa wanakuja kufanya ukaguzi wa jengo ili waulizwe kama hali ya majengo walikuwa wanaiona.

Tukio la ajali ya moto katika shule ya Byamungu Islamic iliyoko wilayani Kyerwa mkoani Kagera, lilitokea usiku wa kuamkia jana Septemba 14, 2020, na kupelekea vifo vya watoto 10 na wengine 7 kujeruhiwa, ambapo bweni hilo lilikuwa na wanafunzi 74.

Lampard afunguka kiwango cha Kepa
Sevilla CF yamnasa Marcos Javier Acuña