Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Siro ameagiza wafanyabiashara na watu wote ambao wanakwepa kulipa kodi nchini kuchukuliwa hatua kali kwani wanarudisha nyuma na kuchelewesha maendeleo ya nchi.

Ameyasema hayo jana alipofanya ziara mkoani Mbeya na kuwaagiza askari wa vikosi mbalimbali vya polisi kuhakikisha wanawakamata na kuwachukulia hatua za kisheria watu wote ambao wanakwepa kulipa kodi.

“Kuna watu wanafikiri ni sifa kufanya magendo wote tunajua umuhimu wa kulipa kodi kwa hiyo tumepanga mpango mkakati wa kuwashughulikia vizuri sana wale ambao wanakwepa kulipa kodi, wananchi wetu wanapaswa kubadilisha mtazamo wao waone wanawajibika kwenye kulipa kodi sababu kodi ndiyo inafanya maendeleo ya nchi yetu, kodi ndiyo inaleta madawa, kodi inaleta barabara na kodi ndiyo kila kitu. Na wale ambao wanakwepa kulipa kodi nimetoa maelekezo kuwashughulikia kila mahali na kila siku wanasikia Amiri Jeshi Mkuu anazungumzia habari hii sasa wewe unayekwepa kulipa kodi ni nani,”amesema IGP Sirro

Hata hivyo, IGP Sirro amewataka wafanyabiashara pamoja na wananchi kulipa kodi ili nchi iweze kupata maendeleo na kusonga mbele zaidi.

France Football waendelea kutaja watakaowania tuzo ya Ballon d'Or
Tume ya haki za binadamu yaibua mapya uchaguzi Kenya