Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amekutana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakati alipomtembelea ofisini kwake Ikulu Zanzibar kwa lengo la kujitambulisha rasmi.

IGP Sirro amefanya ziara ya ukaguzi kisiwani Zanzibar, ziara ambayo imelenga kufanya tathimini ya changamoto na mafanikio wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika visiwani humo.

Akizungumza wakati wa ziara hiyoidha IGP Sirro ameitaka jamii husasani inayoishi katika visiwa vya Unguja na Pemba, kuacha kujihusisha na vitendo vya udhalilishaji kwani Jeshi la Polisi kamwe halitosita kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kuwafikisha mahakamani.

Pia, amekemea baadhi ya vitendo vinavyofanywa na wahalifu wachache wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya na amesema Jeshi la Polisi bado litaendelea kuwashughulikia kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo.

Manara amkingia kifua Mkude
Tetesi za usajili barani Ulaya