Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, ameongezewa mwaka mmoja wa kuendelea  kuongoza Shirikisho la Wakuu wa Polisi Mashariki mwa Afrika (EAPCCO).

IGP Sirro amesema uamuzi huo wa kubakishwa kwenye nafasi hiyo umetokea baada ya kutokumalizia programu zake ikiwemo ya mafunzo ya utayari iliyotakiwa kufanyika Sudan na haikufanyika kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa Covid 19.

“Kutokana na ugonjwa wa Corona uliotokea naona wakuu wa jeshi la polisi ambao ni wanachama wa EAPCCO kila mtu alikuwa anasema programu nyingi sijazimaliza lakini tulikuwa tunataka tuwakabidhi wenzetu wa DRC lakini na nchi hiyo nayo bado haijatulia kwahiyo wameshawishi nibaki kuwa mwenyekiti, ” amesema IGP Sirro.

Sambamba na hilo, IGP Sirro amesema kuna mambo ambayo wamekubaliana kwa mwaka 2020/2021 wayatimize ikiwa ni pamoja na Mafunzo, Oparesheni, kushirikishana taarifa na kutafuta na Magaidi.

TAKUKURU Tanga yaokoa zaidi ya Sh. Millioni 30 za CWT
AU yaikomalia Mali