Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro ametoa maelekezo kwa makampuni ya ulinzi kuacha kuajiri wazee wenye umri mkubwa na kuweka silaha mbili kunapokuwa na walinzi wawili sehemu ya lindo ili silaha moja isaidie kulinda silaha nyingine inapotokea majambazi wamemnyang’anya mlinzi silajha moja.

IGP Sirro ametoa agizo hilo baada ya kukagua kituo cha mafuta Bunju na kugundua uwepo wa uzembe kwa makampuni ya ulinzi kwa kuweka mlinzi mmoja mwenye silaha na mwingine akiwa hana silaha jambo ambalo hutoa mwanya kwa wahalifu kufanya uhalifu.

Aidha amefanya ukaguzi maeneo ya External Ubungo lilipotokea tukio la ujambazi la kumjeruhi mfanyabiashara mmoja kwa risasi na kumsababishia maumivu makali ambapo majambazi hao hawakufanikiwa kuchukua kiasi chochote cha pesa.

Katika ziara yake hiyo ya ukaguzi pia alikagua maeneo ya Mwabepande ambako majambazi walivamia katika kituo cha mafuta (Fuel station) kiitwacho Mexsons Bunju kinachomilikiwa na mfanyabiashara aitwaye SANGA.

IGP Sirro pia amekagua utendaji katika Wilaya ya Kipolisi Mabwepande, Mbweni na kituo cha Polisi Kawena kuongea na wananchi waliokuwa katika vituo hivyo ili kutambua kero zao.

Kesi ya Zuma dhidi ya rushwa yaanza
Uongozi Young Africans washindilia 'MSUMARI'