Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro amesema kuwa lengo la kukutana na viongozi wastaafu wa jeshi hilo ni kutaka kupata ushauri wa namna gani ya kuweza kuliendesha jeshi hilo na kudai kuwa vongozi hao wameona mapungufu mbalimbali ndani ya jeshi hilo ambayo yanatakiwa kufanyiwa marekebisho.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kikao hicho kilichofanyika jijini Dar es salaam, ambapo amesema kuwa kuna mambo kadhaa ameshauriwa na viongozi ambayo linatakiwa kuyafanyia kazi.

“Jambo kubwa ambalo walikuwa wanasisitiza ni suala la weledi kwamba wanapokuwa kule wanatuangalia sisi ambao tuko jeshini tunahudumia Watanzania wanaona kuna mapungufu katika baadhi ya utendaji wa askari wetu, kwa hiyo walikuwa wanasisitiza sana katika suala la weledi, lakini la pili viongozi hawa wanazungumzia sana suala la mafunzo kwamba kila askari anapaswa kuwa na mafunzo mbalimbali,”amesema IGP Sirro

Hata hivyo, Baadhi ya maafisa wastaafu wa jeshi la polisi walioshiriki katika kikao hicho ni pamoja na IGP Mstaafu Ernest Mangu, Said Mwema, Omari Maita pamoja na makamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Suleman Kova na Alfred Tibaigana.

Messi apiga 'Hat-trick' Barcelona ikipaa kileleni
Wapiga dili wa madini wawekwa kikaangoni