Kiungo kutoka nchini Nigeria Victor Ackpan aliyekutana na Thank You ndani ya Simba SC anatajwa kuwa kwenye hesabu za mwisho kujiunga na Ihefu FC.

Ikumbukwe kwamba Ihefu FC ni watibuaji wa rekodi ya Young Africans msimu wa 2022/23 walipogotea kwenye mechi 49 bila kufungwa, walipokutana na Ihefu FC walitibua mpango wao wa kufikia mechi ya 50.

Ni Novemba 29, mwaka 2022 ubao wa Uwanja wa Highland Estate ulisoma Ihefu FC 2-1 Young Africans na rekodi ya kucheza bila kufungwa tangu msimu wa 2021/22 ikagotea Mbeya.

Taarifa zinaeleza kuwa mabosi wa Ihefu FC walitumia muda aliokuwa hapo kwa mkopo kumtazama na kumchuja kwa ukaribu.

“Akpan alikuwa ndani ya Ihefu FC na kwa muda aliokuwa anacheza hapo kwa mkopo akitokea Simba SC alikuwa anaonekana ana kitu, hivyo kama makubaliano yatafikia sehemu nzuri atapewa mkataba,” imeeleza taarifa hiyo.

Simulizi ya Pochettino na usajili Harry Maguire
Pierre Emerick Aubameyang atua Ufaransa