Wakristo kote Duniani leo Aprili 2, 2021 wanaadhimisha ibada maalum ya Ijumaa Kuu kukumbuka mateso ya Yesu Kristo zaidi ya miaka 2000 iliyopita, ambayo yatafuatia na sikukuu ya Ufufuko wa Bwana Yesu Kristo, yaani Pasaka.
Akizungumza na Dar24 Media, Katibu wa Baraza la Maasofu Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima amesema kuwa siku hii ya Ijumaa Kuu ni siku ambayo Yesu anaufia Msalaba ambao ndio Ukombozi na wokovu kwa Wakristo.
Ameongeza kuwa Wakristo wanatakiwa kukumbuka ni jinsi gani Yesu alivyowapenda akitaka wasipotee bali wafikie uzima, ambapo amesema kwa Wakristo leo wanaabudu ule msalaba ulio wakomboa katika dhambi.
Padri Kitima ameongeza kuwa ni vyema mwanadamu kufuata sauti ya Mungu katika roho ili kuwa watu wema na wadumishe mahusiano mazuri.