Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewataka viongozi wa chama hicho kutowaogopa watendaji wa serikali.

Ameyasema hayo wakati wa mkutano mkuu wa tisa wa chama hicho uliofanyika mkoani Dodoma, ambapo amesema kuwa wana CCM wanaruhusiwa kuikosoa serikali.

Amesema kuwa pamoja na kuikosoa serikali pia wanatakiwa wakumbuke kuwa wao ni wana CCM na wanatakiwa wajue namna ya kuikosoa.

“Ndani ya CCM tuna utaratibu wa kukosoana, lakini mnapokuwa mnaikosoa serikali kumbukeni kuna njia nyingi za kuikosoa, na uchungu wa mwana aujuaye mzazi,”amesema JPM

Hata hivyo, Rais Dkt. Magufuli ameongeza kuwa kazi ya chama ni kuwaunganisha wananchi na serikali yao ili waweze kuunganisha nguvu pamoja katika kukuza uchumi wa nchi.

Vanessa Mdee: Maajabu mengi yametokea kwenye maisha yangu
INASIKITISHA: Mtoto aliyefanyiwa oparesheni 10 bila mafanikio atoa neno kwa watanzania (+Video)