Mshambuliaji wa mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba SC Charles Ilanfya, anawaniwa na Mtibwa Sugar, katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili.

Ilamfya ameingizwa kwenye orodha ya wachezaji wanaohitajika Mtibwa Sugar, kufuatia mapendekezo yaliyotolewa na kocha mpya wa klabu hiyo Hitimana Thiery, ambaye ataanza kulikalia benchi la ufundi kwenye mzunguuko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2020/21.

Kocha huyo kutoka nchini Rwanda amethibitiisha kumuhitaji mshambuliaji huyo, ambaye inasemekana atatolewa kwa mkopo na waajiri wake wa sasa (Simba SC), kufuatia kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza, tangu aliposajiliwa mwanzoni mwa msimu huu akitokea KMC FC.

Amesema Ilanfya ni mchezaji nzuri, hivyo ana imani akipata huduma ya nyota huyo atafanya vizuri kwa sababu anafahamu ubora wake mbele ya lango tangu msimu uliopita.

Amesema tayari uongozi wake unafanyia kazi mapendekezo yake ya kupata huduma ya Ilanfya, ambaye amekuwa akitakiwa kwa mkopo na timu nyingi ikiwamo Ihefu FC.

“Niliwaomba nisajili wachezaji watatu, ila nimeona kuna nyota kutoka kikosi cha vijana wa timu hiyo wanafanya vizuri, hivyo nikaomba wazungumze na Simba ili tupate huduma ya Ilanfya.”

“Nimeona safu ya ushambuliaji ni tatizo kubwa, hivyo tukimpata Ilanfya kuja kuongeza nguvu na waliokuwapo ndani ya timu, nina uhakika wakupata matokeo mazuri zaidi,” amesema Hitimana.

Hitimana ambaye amejiunga na Mtibwa Sugar baada ya kuachana na Namungo FC, na kwa bahati mbaya jana aliishuhudia timu yake ikipoteza kwakufungwa 0-1 Dodoma Jiji FC kwenye mechi yao ya kukamilisha mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara.

Kwa matokeo hayo Mtibwa Sugar inaendelea kusalia katika nafasi ya saba na amala zake 22 kwenye msimamo wa Ligi Kuu.

Yondani aibukia Polisi Tanzania
Young Africans yapeta ASFC, Singida Utd yapigwa rungu