Imamu Ramadhani wa Msikiti wa Al Masjid Kirumbi Islamic Center,  uliopo Kimara amewazuia waumini wake kutoshiriki katika kuvunja au kutoa kitu chochote katika msikiti huo ambao unatakiwa kuvunjwa na Wakala wa Barabara Tanzania TANROADS.

Hayo yamesemwa leo wakati akifanyiwa mahojiano na MCL na kudai kutokana na imani yao ni kosa kubwa mtu yoyote kuvunja nyumba ya ibada kwa kuwa hiyo ni nyumba ya Mungu na kusema wao hawajatoa kitu chochote zaidi ya vitu vidogo ambavyo vinatumika kusaidia jamii.

Aidha wamekubali kuwa walipokea barua toka Tanroads kuwataarifu ujio wao unaohusu kuvunja msikiti uliojengwa katika eneo la hifadhi ya barabara.

‘Walitaka tutoe vifaa ndani ya wiki moja kupisha zoezi la barabara lakini kutokana na imani yetu ya Uislamu unavyotufundisha ni kosa kubwa kuvunja nyumba ya ‘Allah Subhanahu Wa Ta’alah’’ amesema Imam Ramadhani.

Pia amesisitiza kuwa dini yao ya kiislamu hairuhusu mtu kwa mkono wake mwenyewe kutoa kitu chochote kile kinachohusu msikiti.

 Hata hivyo Imamu alisisitiza kuwa wao wameiachia serikali na TANROADS waweze kubomoa wenyewe na kusema yeye amewakataza waumini wake wasishiriki cha chochote katika kubomoa nyumba hiyo ya ibada

 

Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 17, 2017
Tanzania na Kenya zashuka viwango vya FIFA, Ujerumani, Brazil za paa juu