Mwanamuziki maarufu wa miondoko Rnb Robyn Rihanna Fenty maarufu kama Rihanna na msanii wa Hip Hop Rakim Mayers maarufu kama A$AP Rocky wapo kwenye mahusiano ya kimapenzi.

Kwa mujibu wa mtandao wa Page Six pamoja na mitandao mikubwa ya habari za burudani nchini Marekani, imeeleza kwamba imewanasa wawili hao wakila chakula cha usiku pamoja.

Rihanna na Rocky walikuwa wakihisiwa muda mrefu kuwa kwenye mahusiano, hii ni tangu Rihanna aachane na bilionea Hassan Jameel mapema mwaka huu.  Ukaribu wao ulianza tangu mwaka 2013.

Hivi karibuni walishirikiana kwenye kampeni ya Fenty Skin line na walifanya mahojiano na Jarida la GQ na Vogue kwa ajili ya promosheni.

Serikali yatenga Bil. 4 kuimarisha miundombinu Jangwani
Simba SC yaikasirisha TFF