Mkazi wa kijiji cha Nyang’oma Mkoani Mara, anayejulikana kwa jina la Nyandaro Kusoya anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuichoma moto mikono ya mtoto wa kaka yake, Sarah Kaela.

Kamanda wa polisi Mkoani humo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo mtuhumiwa huyo mwenye umri wa miaka 29 alimchoma mtoto Sarah mwenye umri wa miaka mitatu kwa kile alichodai kuwa alifanya kosa la kulamba sukari.

Bibi wa mtoto huyo Nyamata Chihoye amesema mtuhumiwa huyo Nyandaro Kusoya alimfata mjukuu wake huyo  na kuondoka naye kwa lengo la kwenda kuishi naye katika kijiji cha Nyang’oma Musoma vijijini Mkoani Mara na matokeo yake kusikia mjukuu wake amefanyiwa kitendo cha kikatili.

Aidha, Kamanda Mohamed amesema wanafanya taratibu za kisheria ili kuhakikisha wanamfikisha mtuhumiwa mahakamani.

 

Kanisa Katoliki limelaani kuzuiliwa kwa maandamano
Video: Prof. Beno Ndulu aaga, Kura ya CCM yaipa Ukawa ushindi