Kijana mmmoja mwenye umri wa miaka 25, mkazi wa Bangladesh nchini India amekubwa na ugonjwa wa ajabu baaada ya kupata virus vinavyofahamika kama ‘Human Pappiloma’ unaosababisha ugonjwa wa ngozi na kusababisha kuota vitu mithili ya mizizi ya mti mikononi na miguuni.

 

Abul Bazadar, ambaye alikuwa anafanya kazi ya udereva, amelazwa katika hospitali ya Dhaka, Bangladesh baada ya kuzidiwa. Wazazi wake wameeleza kuwa kijana wao alipata virus hivyo tangu akiwa na umri wa miaka 10. 

Mgonjwa2

Mratibu Mkuu wa taasisi ya upasuaji ya taifa nchini humno inayojulikana kama ‘National Institute of Burn and Plastic Surgery’, Dk. Samatha Lal Sen, aliwaambia waandishi wa habari kuwa madaktari wataamua namna ya kumtibu baada ya kuunda Bodi ya jopo la madaktari kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Abul Bazadar akiwa na familia yake

Abul Bazadar akiwa na familia yake

Dunia ina magonjwa mengi ya ajabu, tuombaeni na tushukuru kwa kila jambo.

 

My Story: Nilivyojikuta Naupenda ukimwi alioupata mpenzi wangu na kilio chake
Facebook, Instagram wapiga marufuku matangazo ya Bunduki