Sheria kali za Indonesia zilizomkuta na hatia mwanamke mmoja kwa kosa la kufanya mapenzi nje ya ndoa yake zimemgharimu mwanamke huyo akiwa anapewa adhabu ya viboko mbele ya umma.

Indonesia 2

Kwa mujibu wa DailyOnline, mwanamke huyo alifikishwa katika jukwaa lililoandaliwa kutolewa adhabu huko Banda Aceh akiwa amefunikwa usoni na kulazimishwa kupiga magoti na askari wawili kabla ya kuanza kutandikwa viboko kwa idadi iliyotolewa na mahakama nchini humo.

Hata hivyo, kipigo hicho cha viboko kilimzidia mwanamke huyo na kusabisha aanguke ghafla na kupoteza fahamu baada ya kumaliza adhabu na kisha kuondolewa kwenye eneo la hilo akiwa amebebwa kwenye machera.

Indonesia 3

Wakati mwanamke huyo akipata adhabu, wanaume wengine wawili, mmoja akiwa anatembea kwa msaada wa ‘magongo’, walikuwa wakisubiri kupewa adhabu kama hiyo kwa kosa la kufanya mapenzi nje ya ndoa.

Indonesia 4

Mwezi uliopita, serikali ya Indonesia ilipiga marufuku raia wake kuadhimisha sherehe za Valentine wala kupeana zawadi zinazoashiria sherehe hizo kwa madai kuwa ni kinyume cha sheria za nchi hiyo.

Lil Kim atangaza rasmi ujio wake mpya
Chadema waponea ChupuChupu kuvurugana?