Maisha ya Mariam, msichana mwenye umri wa miaka 16 anayesoma kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Kawe Ukwamani, maisha yake yako hatarini kutokana na ugonjwa unaofahamika kitaalam kama ‘Intestinal Obstruction’. Ugonjwa huu husababisha utumbo kuziba na kushindwa kupitisha chakula.

Hadi sasa Mariam amefanyiwa upasuaji wa tumbo mara kumi (10) bila mafanikio. Mtoto huyu anatakiwa kupata matibabu ya haraka nchini India, lakini hali ya maisha ya wazazi wake haimudu gharama za matibabu hayo, kwani jumla ya gharama za matibabu pamoja na msindikizaji mmoja ni shilingi milioni 40 (TZS).  Kadiri siku zinavyokwenda, hali ya mtoto Mariam inazidi kuwa mbaya.

Video: Maelezo mafupi ya mtoto Mariam Ibrahim Mwema

Mimi na wewe ni tunaweza kuwa chanzo kikuu cha kurejesha furaha na uzima wa mtoto Mariam. Mariam hawezi kula, maisha yake yamejaa maumivu makali muda wote.

Hivyo, anahitaji msaada wako ili akapate matibabu haraka mchini India, gharama ya matibabu ni shilingi milioni 40 za kitanzania.

Tafadhali, tunaomba tuma mchango wako sasa kupitia Tigo Pesa, M Pesa, Airtel Money. Namba ya Kampuni ni 400700, Namba ya kumbukumbu 400700. Utakuwa umesaidia kuokoa maisha ya Mariam. 

Kutokana na maradhi yanayomkabili, Mariam ameshindwa kufanya mtihani wake wa kuhitimu masomo ya sekondari ( kidato cha nne) mwaka huu, akiuguza mishono ya upasuaji, maumivu makali na kutumia muda mwingi hospitalini. Ndoto yake kubwa ya kujiunga na taaaluma ya udaktari inafifishwa na ugonjwa huu.

Video: Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema ameguswa na tatizo la Mariam na kuwaomba Watanzania kuokoa maisha ya Mariam

“Nikipona nitajitahidi kutimiza ndoto yangu ya kuwa Daktari Bingwa wa kitengo cha upasuaji ili niwasaidie pia wenye tatizo kama langu na matatizo mengine ya afya. Naomba kila Mtanzania na asiye Mtanzania naamini ameguswa, anisaidie nipate matibabu ili niendelee kuishi. Ninaumia sana,” Mariam ameiambia Dar24.

“Ombi langu kubwa kwa Mwenyezi Mungu ni kuwa mzima. Naamini Mungu atawatumia Watanzania wenzangu na madaktari kuniponya na wao watabarikiwa sana. Naomba nisaidieni, napenda kuishi pia,” aliongeza.

Video: Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa ameguswa na tatizo la Mariam na kuwaomba Watanzania kuokoa maisha ya Mariam

Shiriki baraka hizi, hakuna lililo jema na lenye kheri zaidi duniani kama kuokoa maisha ya mwenzako. Tafadhali, toa chochote ulichonacho kadiri ulivyoguswa na uwezo wako, utazidishiwa kwa kurejesha afya na kuokoa maisha ya mtoto Mariam.

TUKO PAMOJA #OkoaMaishaYaMariam Tusikubali kumpoteza Mariam

Kwa mawasiliano zaidi tupigie kupitia: 0679 979 786 au +255 222 701 845/6
Email: info@dar24.com

Video: Maelezo kamili kuhusu ugonjwa unaomtesa mtoto Mariam yalivyotolewa na mama yake Mariam pamoja na Mariam mwenyewe, ‘INAUMA SANA

Ikosoeni serikali kwa utaratibu- JPM
Video: Ni Magufuli, Vigogo watano watumbuliwa NHC