Nchi ya India imerekodi ongezeko kubwa la visa vya maambukizi ya virusi vya Corona kwa siku moja jana Jumatatu wakati serikali ikianza kuchukua hatua ya kulegeza masharti yaliyowekwa kuzuia maambukizi.

Katika kipindi cha saa 24 India imerekodi kesi 1,553 za maambukizi na kufanya idadi jumla ya walioambukizwa virusi vya Corona nchini humo kufikia watu 17,000.

Serikali ya nchi hiyo iliamua kulegeza masharti ili kuruhusu shughuli za utengenezaji bidhaa na kilimo kuanza kazi.

Watatu wafariki kwa Corona Dar

Takriban watu 543 wameshakufa kutokana na ugonjwa wa Covid-19 nchini humo na wataalamu wa magonjwa ya mlipuko wametabiri kwamba kilele cha maambukizi nchini India kitafikiwa mwezi Juni.

Video: Kifo cha Mchungaji Rwakatare chatikisa, Serikali yatoa ahueni barakoa
Watatu wafariki kwa Corona Dar