India imesema imekubaliana na China kushughulikia mgogoro uliopo katika mpaka unaotenganisha mataifa hayo mawili kwenye mkutano baina ya mawaziri wa ulinzi wa nchi zote mbili.
Waziri wa Ulinzi wa India Rajnath Singh na mwenzake wa China Wei Fenghe wamekutana pembeni ya mkutano wa shirika moja la shangai, Mocow jana jioni.
Pande zote mbili kupitia Himalaya magharibi zimepeleka vikosi vya ziada, kando ya mipaka yake baada ya mvutano wa mwezi Juni ambapo wanajeshi 20, wa India waliuawa katika mapigano.China haijaripoti takwimu zozote za kujeruhiwa kwa vikosi vyake.
Waziri wa ulinzi wa India amesema wamekubaliana kuwa upande wowote usichukue hatua ambayo inaweza kuhatarisha hali zaidi katika maeneneo ya mpakani.
Huo ni mkutano wa ngazi ya juu zaidi wa uso kwa uso katika siasa za China na India tangu kutokea kwa mzozo kando ya mlima uliopo mpakani mwa mataifa hayo mawili.