Maambukizi a virusj vya corona nchini India yamefikia Milioni 25, ikiwa ni taifa la pili ulimwenguni kufikia idadi hiyo baada ya Marekani.

Visa vipya 263,533 vimerekodiwa katika saa 24 zilizopita na kupelekea jumla ya maambukizi kuwa Milioni 25.23.

Idadi ya maambukizi mapya imekuwa ikipungua katika Taifa hilo ambalo Hospitali zimekuwa zikilazimika kukataa wagonjwa.

Tangu Aprili 21, visa visivyopungua 300,000 vimekuwa vikirekodiwa.

Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya nchini humo, jumla ya idadi ya waliofariki dunia kuokana na covid-19 imefikia 278,719 baada ya vifo 4,329 kurekodiwa ndani ya siku moja.

Rasmi Ariana Grand afunga ndoa
Sheria ya PF3 itazamwe upya- Rais Samia