Nchi ya India imesitisha uagizaji wa vifaa vya kupimia virusi vya corona kutoka China baada ya kubainika kuwa vifaa hivyo havina ubora unaotakiwa.
Hatua hiyo imeenda sambamba na kuondoa vile ambavyo vilisambazwa kwenye majimbo kadhaa ambapo, mji wa Delhi pia umeondoa vifaa ambavyo tayari vilikuwa vinatumika.
Vifaa hivyo huchukua muda wa karibu dakika 30 kutoa majibu. Hutumiwa kusaidia maafisa kuelewa hali ya maambukizi katika eneo fulani.
Awali mamlaka nchini humo, ICMR ilikua ikikataa, lakini ilifungua milango, kuingiza vifaa vya upimaji kutoka kwa makampuni mawili ya nchini China.
Hatahivyo, muda mfupi baada ya majimbo kadhaa kuanza kulalamika kuwa vifaa hivyo vya kupimia vina uhakiki wa 5% pekee, yakiongeza kuwa yalivitumia kwa wagonjwa ambao tayari walishafahamu kuwa wana maambukizi , lakini majibu yalionekana hawajaambukizwa.
maafisa wameviambia vyombo vya habari nchini humo kuwa serikali ”haitapoteza hata rupia moja” kwa kuahirisha kuagiza vifaa hivyo kwa kuwa hawajailipa China malipo ya awali, na kufunga kabisa zoezi la uingizaji wa vifaa hivyo nchini India.