Wizara ya Afya ya India, imerekodi maambukizi mapya ya Virusi vya Corona 103,558, hii ikiwa ni idadi kubwa zaidi kurekodiwa katika siku moja.

Visa vya Virusi vya Corona nchini humo vimefikia Milioni 12.6 huku waliofariki dunia wakifikia 165,101 baada ya ongezeko la vifo 478.

Jimbo la Maharashtra ambapo Jiji la Mumbai linapatikana limetajwa kuathirika zaidi, huku takriban nusu ya maambukizi mapya yakitokea huko.

Serikali ya Jimbo hilo imetangaza kanuni mbalimbali kudhibiti mlipuko ikiwemo ‘Lockdown’ mwishoni mwa wiki.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Aprili 6, 2021
Rais Samia atengua uteuzi wa Mkurugenzi aliyemteua jana