Raisi wa shirikisho la soka duniani FIFA Gianni Infantino amesema wachezaji Marcus Thuram wa Borrusia Monchengladbach, Jadon Sancho na Achraf Hakim wa Borusia Dortmund hawapaswi kuadhibiwa na Chama Cha soka nchini Ujerumani kwa kosa la kuunga mkono waandamanaji nchini Marekani kupinga mauaji ya mtu mweusi George Floyd.
Infantino amesema moja ya kauli mbiu ya FIFA Ni kupiga vita dhidi ya ubaguzi wa rangi, na ndio maana wana kauli mbiu ya (SAY NOT RACISM) na kilichofanyika KWA George ni ubaguzi huo huo.
Sancho na Hakim walionyesha jezi zao zikiwa na maandishi ya kuunga mkono waandamanaji kupinga ubaguzi dhidi ya weusi na kudai haki “JUSTICE FOR GEORGE FLOYD”.
Raisi Infantino amesema watu hao wanapaswa kupongezwa sio kuadhibiwa.
Thuram alipiga goti kuashiria kuunga mkono waandamanaji nchini Merakani.
Uongozi wa chama cha soka nchini Ujerumani DFB, ulisema unachunguza uwezekano wa kuwapa adhabu wachezaji hao au vinginevyo.