Nahodha wa timu ya taifa ya Uswiz, Gokhan Inler amewatahadharisha wachezaji wenzake kuwa makini na kutodharau mchezo wa hii leo ambao unakwenda kuwakutanisha dhidi ya England kwenye uwanja wa ugenini huko jijini London.

Inler ametangaza tahadhari hiyo kwa wenzake kufuatia mtazamo wa kundi la tano kuonyesha tayari nchi hizo mbili zimeshafanikiwa kufuzu kucheza fainali za mataifa ya barani Ulaya za mwaka 2016.

Inler ambaye anaitumikia klabu ya Leicester City, amesema itakua ni upuuzi na uwendawazimu kwa wachezaji wa timu ya taifa ya Uswiz kucheza mchezo wa hii leo kwa kujishusha na kuamini hakuna athari zozote kwa kisingizio cha kufuzu kucheza fainali za mwaka 2016.

Amesema mapambano bado yanaendelea na dhamira iliopo sasa ni kuhakikisha wanashinda michezo yote iliyobaki ili kudhihirisha ubora wao katika mipango waliyokua wamejiwekea tangu mwanzo wa kampeni za kusaka nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya barani Ulaya ambazo zitaunguruma nchini Ufaransa mwaka ujao.

Uswiz wapo katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi la tano kwa kumiliki point 15 huku wapinznai wao England wakiwa kileleni baada ya kuzinyakua point 21 huku wakiwa na uwiyano mkubwa wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliozikutanisha timu hizo mjini Basel kwenye uwanja wa St Jacob, England walifanikiwa kuchomoza na ushindi wa mabao mawili kwa sifuri yaliyofungwa na mshambuliaji wa Arsenal, Danny Welbeck.

Sauti ya Barnaba Kusambaza Injili’
Pizarro Arejea Werder Bremen