Bao lililofungwa na kutoka nchini Colombia Fredy Alejandro Guarín Vásquez,  lilitosha kuipa point tatu klabu ya Inter Milan ambazo zimeipeleka kileleni mwa msimamo wa ligi ya nchini Italia Serie A.

Fredy Guarin alifunga bao hilo katika mchezo muhimu dhidi ya mahasimu wa Inter Milan, AC Milan ambao walionekan kuwa katika hali ya simanzi mara baada ya kipyenga cha mwisho kupulizwa.

Kikosi cha Inter Milan chini ya utawala wa meneja Roberto Mancini kilionyesha kuwa katika hali ya ukomavu wa kimapambano kwenye mchezo huo na ilidhihirika mambo yengekua mazuri mwishoni mwa dakika 90 kutokana na soka safi walilokua wakicheza.

Mashabiki wa soka wa mjini Milan walipata fursa ya kumshuhudia mshambuliaji Mario Balotelli aliyesajiliwa na AC Milan kwa mkopo akitokea Liverpool akicheza kwa mara ya kwanza kwenye uwanja wa San Siro tangu alipoondoka mwezi August mwaka 2014, lakini alishindwa kuisaidia klabu yake.

Ushindi huo wa bao moja kwa sifuri umeiwezesha Inter Milan kufikisha point 9 baada ya kushinda michezo mitatu mfululizo tangu kuanza kwa ligi ya nchini Italia msimu wa 2015-16.

Michezo mingine iliyochezwa jana katika ligi hiyo ilishuhudia.

Hellas Verona 2 – 2 Torino

Empoli 2 – 2 SSC Napoli

Palermo 2 – 2 Carpi

Sassuolo 2 – 2 Atalanta

Lazio 2 – 0 Udinese

Ufisadi Wa Jack Warner Waendelea Kudhihiri FIFA
Ndoa Ya Spurs Na Adebayor Yavunjika Rasmi