Uongozi wa klabu ya Inter Milan ya Italia imetangaza maamuzi mapya iliyofikia kwa beki wa zamani wa Man United aliyejiunga na Inter Milan mwaka 2014 Nemanja Vidic.
Inter Milan wametoa waraka huo January 18 kuwa wamevunja mkataba na beki huyo wa kimataifa wa Serbia. Inter Milan wamefikia maamuzi ya kuvunja mkataba na Vidic baada ya kufanya mazungumzo na mchezaji huyo na kufikia makubaliano, Vidic ambaye amejiunga na klabu ya Inter Milan mwaka 2014 akitokea Man United alikodumu kwa miaka nane, ameshindwa kutamba na Inter Milan baada ya kuandamwa na majeruhi kila wakati.
Vidic akiwa ndani ya Inter Milan amefanikiwa kuitumikia michezo 28 msimu uliopita, wakati akiwa Man United anahesabika kama nguli, akiwa ndani ya Man United Vidic amecheza jumla ya mechi 300 katika kipindi cha miaka nane na amefanikiwa kutwaa mataji 10 ila ameshindwa kutamba na Inter kutokana na majeruhi.

Zari na Wema Sepetu wapeana 'Makavu' kwenye mtandao
Utafiti: Vijana wasema watampigia kura mgombea atakayewapa rushwa