Kampuni inayoongoza kwa kutoa huduma ya Fiber (FTTH) Zuku Fiber imezindua intrernet yenye kasi zaidi kupitia vifurushi vyake ambavyo imekuwa ikitolea huduma hiyo.
Uzinduzi huo umefanyika hii leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Zuku Fiber, Thomas Hintze, ambapo amesema kuwa internet yenye kasi zaidi Tanzania itawasaidia wananchi kupitia fursa mbalimbali.
“Huduma hii ambayo tunaizindua leo ni msaada mkubwa sana kwa watumiaji wa mitandao kwani ina kasi kubwa sana ni huduma ya kisasa ambayo itaboresha huduma zao,”amesema Hintze.
Amesema kuwa ili kukidhi mahitaji ya watumiaji wa internet, kampuni hiyo imeanzisha vifurushi mbalimbali vya huduma nafuu ikiwa ni pamoja na 10Mbps, 20Mbps na kifurushi cha 40Mbps.
-
Video: Makonda azidi kuiboresha Dar, biashara ya magari kufanyika Kigamboni tu
-
Watumishi wa umma waonywa kuhusu taarifa za Serikali
-
Video: Jeshi la Polisi lakanusha Askari wake kumfuata Tundu Lissu Kenya
Hata hivyo, ameongeza kuwa watumiaji wa internet wataweza kunufaika na bidhaa mbalimbali zitokanazo na kampuni hiyo.