Abel Paul, Jeshi la Polisi – Dar es Salaam.

Taasisi ya Mahusiano ya Umma Tanzania – IPRT, imehitimisha mafunzo ya siku tano ambayo yalianza Oktoba 2-6, 2023 kwa kundi la Maafisa na Wakaguzi Wanafunzi 953 wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam – DPA.

Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam Kamishna msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP Dkt. Lazaro Mambosasa amesema mafunzo hayo ya kimkakati ya Mawasiliano, yamelenga kuwajengea uwezo wa kiutendaji pindi watakaporejea makazini na kutoa huduma bora kwa Wananchi.

Amesema, imekuwepo dhana hasi katika mawasiliano baina ya Jeshi hilo na wananchi na kuwataka Maafisa hao kwenda kubadilisha dhana hiyo yalete tija kiuchumi kwa Watanzania pale watakapoweza kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu katika maeneo tofauti tofauti hapa nchini.

Kwa upande wake Mkurungezi wa Taasisi ya Mahusiano ya Umma Tanzania – IPRT, Dkt. Gabriel Nderumaki amesema kuwa mafunzo hayo yamelenga kuwaongezea uwezo wa mawasiliano ya kimkakati na kwamba Taassisi hiyo itaendelea kushirikiana na Jeshi hilo katika kuwaongezea uwezo wa kimawasiliano.

Naye Mratibu wa mafunzo wa Taasisi ya Mahusiano ya Umma Tanzania – IPRT, Bi. Elizabeth Wachuka ameseama jumla ya mawasilisho 26 yalitolewa na kugawanywa katika makundi matatu ambayo ni mawasiliano, uongozi huku akibainisha kuwa kundi lingine lilizingatia mafunzo ya Jeshi la Polisi yaliyotolewa na maafisa Wastaafu wa Polisi.

Luis Enrique: Ninastahili kulaumiwa
Sheria uhuru wa Vyombo vya Habari ni muhimu - Dkt. Mzuri