Mwanafunzi ambaye video yake ilisambaa katika mitandao ya kijamii akilalamikia kubadilishiwa namba ya mtihani na baadaye mamlaka kufuatilia ukweli, amepata alama ya wastani wa A kwenye matokeo yake ambayo yametangazwa na Baraza la Mtihani Tanzania (NACTE).

Mwanafunzi huyo, Iptisam Suleiman Slim wa Shule ya Msingi Chalinze Modern Islamic ‘Pre and Primary School’ amefaulu kwa wastani wa A katika matokeo ya Darasa la Saba yaliyotangazwa na NECTA hii leo Desemba Mosi, 2022 ambapo mtihani wa kumaliza elimu ya msingi ulifanyika Oktoba 5 na 6, 2022.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda (kushoto) akizungumza na Mwanafunzi Iptisam Suleiman Slim (katikati) na mzazi wake ambapo awali alisema atawachukulia hatua wasimamizi wa mitihani kituo hicho na kumuagiza mwenye Shule kuwafukuza wote waliohusika na udanganyifu.

Iptisam mwenye namba ya mtihani (PS1408009-0039), amefaulu Kiswahili kwa kupata alama A, English A, Maarifa A, Hisabati B, Sayansi A na Uraia B akiwa na wastani wa A, huku ikukumbukwa kwamba Serikali iliifungia shule yake kuwa kituo cha mitihani kwa muda usiojulikana kutokana na sakata hilo.

Oktoba 25, 2022, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda alisema taarifa ya Kamati ya Mitihani ya Mkoa wa Pwani pamoja na taarifa ya Wataalam wa Miandiko (Forensic Bureau) kutoka Jeshi la Polisi nchini, ilibainika kuwa jumla ya watahiniwa saba walibadilishiwa namba za mtihani katika kituo PS1408009 shule ya Awali na Msingi Chalinze Modern Islamic.

Kocha Mexico akubalia yaishe, aachia ngazi
Tshisekedi anatumia mgogoro kuchelewesha uchaguzi: Kagame