Rais Donald Trump wa Marekani anatarajiwa kutangaza iwapo ataachana na mkataba wa nyuklia wa Iran, huku rais wa Iran akionya kuhusu uwezekano wa nchi hiyo kupitia kipindi kigumu kufuatia maamuzi yatakayotolewa na Trump.
Rais Trump anatarajiwa kutangaza maamuzi hayo baadae hii leo, ambapo Mkataba huo ulifikiwa chini ya mtangulizi wake Barack Obama, kwa ushirikiano na China, Urusi, Ujerumani, Ufaransa na Uingereza ulikuwa na lengo la kuleta nafuu ya vikwazo dhidi ya Iran.
Kwa upande wake, Rais wa Iran, Hassan Rouhani ameonya kuhusu uwezekano wa taifa hilo kupitia katika kipindi kigumu, baada ya maamuzi hayo ya Marekani.
Hata hivyo, Rouhani ameongeza kuwa Iran inataka mahusiano yenye tija na ulimwengu, lakini itaendeleza maendeleo ya ndani licha ya vikwazo vinavyotarajiwa dhidi yake kutoka Marekani.