Serikali nchini Iran imezindua mfumo mpya na wakisasa wa kujilinda kwa makombora unao weza kulenga shabaha sita kwa adui kwa wakati mmoja.
Mfumo huo ulio tengenezwa nchini humo ,umepewa jina la khordad 15 umezinduliwa mbele ya waziri wa ulinzi wa Iran, Brigedia Jenerali Amir Hatami.
Imeelezwa kuwa mfumo wa makombora hayo una uwezo wa kugundua ndege za kivita na droni kutoka umbali wa kilomita 150 na kuzifuatilia katika umbali wa kilomita 150.
Uwezo mwingine mkubwa ambao mfumo huo unao ni kugundua maeneo ya siri na kuyasambaratisha katika umbali wa kilomita 45 na unatumia makombora ya sayyad 3.
Mbali na hayo nchi ya Iran imeelezwa kuwa uwezo wake wa kijeshi ni kwaajili ya kujilinda pekee na sio kuwa tishio kwa nchi nyingine.