Muigizaji wa Bongo Movie, Irene Uwoya hatimaye amefanikiwa kupata tiketi ya kuingia bungeni baada ya kushinda katika mchakato wa kumpata muwakilishi wa Viti Maalum Taifa kupitia CCM.

Uwoya amethibitisha taarifa hizo jana kwa furaha wakati akiongea na kipindi cha XXL cha Clouds Fm.

“Niliweka mtu wa kunihesabia kura lakini tukafungana, tukajikuta watu wawili tumefungana lakini baadaye hatukutangaziwa majibu kwasababu kamati zilikuwa hazijakaa kuamua kwahiyo sasa hivi ndio nimepata majibu,” amesema.

“Tabora nilipita kwa kura nyingi sana na huku taifa pia nimepita kwahiyo namshukuru Mungu.”

Hatimaye Octopizzo Awashinda Dr. Dre Na Beyonce, Avunja Rekodi iTunes
ITV na Radio One wapewa Onyo