Serikali Mkoani Iringa kwa kushirikiana na Vyuo vikuu vilivyopo mkoani humo wanatarajia kufanya tafiti zitakazowawezesha kupata majibu ya tatizo la Utapiamlo ambalo limekua likiathiri watoto wengi licha ya kuzalisha ya wakazi wake kuzalisha chakula kwa wingi.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Halima Dendego wakati akifanya mahojiano maalum na Dar24 ofisini kwake am APL amesema tayari wameanza mchakato wa suala hilo baada ya kuongea na Vyuo hivyo vikuu kikiwemo cha Tumaini.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Halima Dendego.

Amesema, “Hili jambo hata mimi  linanishangaza maana Mkoa wa Iringa unazalisha chakula kwa wingi na inakuwaje watoto wanakumbana na adha hii, sasa moja ya hatua ambazo tumeanza kuchukua in pamoja na utafiti.

Aidha, Mkuu Hugo wa Mkoa pia amesema pamoja na utafiti huo pia wanatarajia kupambana na vitendo vya kikatili ambavyo vimekuwa vikitokea katika maeneo mbalimbali huku akisisitiza suala la kuwashughulikia wait wenye kujihusisha na matukio ya uvunjifu wa amani.

Changamoto za jamii zitaondoshwa na wanajamii: Kasesela
Mbunge achangia ujenzi shule ya Kiislam