Mshambuaji wa Nigeria Isaac Promise amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 31.

Taarifa iliyothibitishwa na klabu yake ya Austin Bold ya Marekani, imeeleza kuwa, Promise alifikwa na umauti usiku wa jumatano, lakini mpaka sasa chanzo cha kifo chake hakijaelezwa.

Promise alikiongoza kikosi cha Nigeria kama nahodha, wakati wa michuano ya Olimpiki 2008 iliyofanyika Beijing, China, na kufanikiwa kuwa sehemu ya wachezaji waliovishwa medali ya fedha, baada ya timu hiyo kumaliza kwenye nafasi ya tatu.

Muda mwingi wa maisha yake ya kucheza soka aliutumia akiwa Uturuki na klabu za Trabzonspor na Antalyaspor, na baadae alijiunga na Al-Ahli ya Saudi Arabia kabla ya kwenda Marekani.

Aliyekua beki wa West Ham United Anton Ferdinand, amekua mmoja wa wanasoka waliotuma salamu za rambirambi, kufuatia msiba wa Promise.

“Nimeshtushwa,” Ameandika mkongwe huyo kupitia Instagram.

“Ulikua mwenzangu na tumeishi chumba kimoja tukiwa Antalyaspor. Pumzika kwa amani Isaac Promise. Pumzika kaka.”

RC Chalamila awasimamisha shule wanafunzi wote kidato cha 5 na 6
Tanzania: Wakimbizi 600 wa Burundi warudishwa kwao