Kiungo wa klabu ya Real Madrid, Francisco Roman Alarcón Suárez maarufu kama Isco amekubali kuongeza mkataba wa miaka mitano utakaomfanya kubaki katika klabu hiyo mpaka ifikapo mwaka 2022.
Real Madrid wanatambua kuwa Isco ambaye kwa sasa anacheza kwa kiwango cha juu mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu na angeweza kuondoka huru katika klabu hiyo.
Isco mwenye umri wa miaka 25 alichukua nafasi ya Gareth Bale aliyepata majeraha msimu uliopita akifunga mabao 10 katika michezo 30.
-
Paul Pogba huenda akawa nje ya uwanja kwa zaidi ya mwezi
-
Jorge Celico abebeshwa zigo la kufuzu kombe la dunia
-
Dimitry Seluk kumtibua tena Guardiola?
Mpaka sasa Isco ameichezea Madrid michezo 7 msimu huu na anweza kuwa miongoni mwa kikosi cha Real Madrid kitakachochuana na Real Sociedad siku ya Jumapili.
Mkataba mpya wa Isco utamfanya kubaki katika klabu ya mabigwa hao watetezi wa michuano ya klabu bingwa Ulaya mpaka tarehe 30 mwezi Juni mwaka 2022.