Klabu ya Arsenal inaendelea kuhusishwa na mpango wa kutaka kumsajili kiungo kutoka kwa mabingwa wa Hispania Real Madrid Isco.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28, anahusishwa na mpango wa kuelekea kaskazini mwa jijini London, wakati wa usajili wa dirisha dogo la usajili ambalo rasmi litafunguliwa mapema juma lijalo (Mwezi Januari 2021).

Isco amekua muhanga wa kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Real Madrid kinachonolewa na Zinedine Zidane, hali inayoendelea kumpa matamanio ya kuhitaji kuondoka, ili apate nafasi ya kucheza mara kwa mara.

Wakati huo huo Kiungo wa kati kutoka nchini Uholanzi Georginio Wijnaldum mwenye umri wa miaka 30, ataamua ndani ya juma hilo iwapo atasaini mkataba mpya wa kuendelea kuwatumikia mabingwa wa soka nchini England Liverpool FC ama kuondoka.

Kiungo huyo yupo njia panda katika kufanya maamuzi hayo, kufuatia kuhusishwa na mpango wa kuhitajika kwenye kikosi cha FC Barcelona, kinachonolewa na meneja kutoka nchini Uholanzi Ronald Koeman.

Koeman anatumiwa kumshawishi kiungo huyo, kujiunga naye huko Camp Nou, ili kuongeza nguvu kwenye kikosi cha Barca ambacho msimu huu, kimekua na wakati mgumu kiushindani kwenye Mshike Mshike wa ligi ya Hispania (La Liga).

Ndugulile aifunda TPC, aipa siku 90
KMC FC kuifuata Mbeya City