Kiungo Mshambuliaji wa PSG, Neymar Jr ambaye anahusishwa na tetesi za kujiunga na Manchester United, imethibitika taarifa hizo sio kweli kama ambavyo zilizuka siku mbili zilizopita.

Neymar Jr ambaye amekuwa na majeraha kwa miezi kadhaa ndani ya PSG alihusishwa na kujiunga na United, lakini kwa mujibu wa taarifa ya klabu yake iliyonukuliwa na ESPN imesema hakuna majadiliano yeyote baina ya mchezaji huyo na wababe hao wa soka wa pale kwenye dimba la Old Trafford.

Winga huyo wa kimataifa wa Brazil inaelezwa hana furaha ndani ya miamba ya soka wa Ufaransa, jambo ambalo linaelezwa afikirie kuondoka mwishoni mwa msimu huu.

Taarifa kwa mujibu wa ripoti hiyo, hata kama Neymar ataondoka PSG, lakini hakuna mpango wowote uliowazi atatua Manchester United.

Taarifa kutoka PSG zinaeleza klabu hiyo inafanya mazungumzo kwa ajili ya kuachana na Neymar Jr kwenye dirisha kubwa lijalo majira ya joto, kwa sababu haipendezwi na mwenendo wa mchezaji huyo.

Mapema mwezi uliopita mashabiki wa PSG walikusanyika nje ya nyumba ya Neymar na kumtaka aondoke kwenye klabu yao.

Ugonjwa uliouwa wawili Rombo hauhusiani na Kimeta - Dkt. Lutege
Wanawake wenye ndoto za uongozi watakiwa kuongeza ujasiri