Kundi la kigaidi linalojiita Islamic States of Iraq and Iran (ISIS), limetajwa kuhusika na tukio la bomu la kujitoa mhanga lililochukua uhai raia wa kigeni zaidi ya kumi katika eneo moja la watalii jijini Istanbul nchini Uturuki, Jumanne wiki hii.

Ingawa hakuna kundi lolote lilojitokeza na kudai kuhusika na tukio hilo, Waziri Mkuu wa Uturuki, Ahmet Davutoglu amesisitiza kuwa kundi la ISIS ndilo lilohusika kutokana na upelelezi uliofanywa na nchi hiyo.

Serikali ya Uturuki imeiambia CNN kuwa katika tukio hilo, Wajerumani 9 waliuawa na watu wengine 15 walijeruhiwa vibaya.

“Hawakuwalenga waliokufa pekee. Waliwalenga Uturuki yote na dunia nzima,” alisema Davutoglu.

Chancellor wa Ujerumani, Angela Merkel alitahadharisha kuwa idadi ya waliopoteza maisha katika tukio hilo inaweza kuongezeka.

 

Bulembo: uchaguzi wa marudio Zanzibar utakuwa huru na haki kama ule ulivyopita
Jurgen Klopp Ashangazwa Na Meneja Wa Arsenal