Kundi la kigaidi la ISIS juzi limetuma ujumbe mpya kwa serikali ya Urusi kupitia kipande cha video kinachoonesha wakimuua kikatili kwa kumchinja mpelelezi wa Urusi.

Katika kipande hicho cha video, kundi hilo limetangaza vitisho vya kufanya mashambulizi katika jiji la Moscow nchini Urusi na New York nchini Marekani kwa lengo la kulipa kisasi kwa mashambulizi yanayofanywa na nchi hizi dhidi yao.

Mpelelezi huyo wa Marekani ambaye jina lake halikutajwa, alidaiwa kuwa aliingia nchini Syria mwaka 2014 kufanya kazi.

“Tutawauwa watoto wenu kwa kila mtoto mliyemuua hapa. Na tutavunja nyumba zenu kwa kila nyumba mliyovunja hapa,” alisema mwanajeshi wa ISIS kwenye video hiyo.

Serikali ya Marekani tayari imeeleza kuwa inaweza kulitokomeza kundi hilo ndani ya miezi michache.

‘Ander Herrera, Marouane Fellaini lazima Waondoke Old Trafford’
Ronda Rousey na Holly Holm Kuzichapa Tena