Rais wa Marekani, Donald Trump ametangaza kujitoa katika mkataba wa kimataifa wa Nyuklia wa Iran, ambapo amesema kuwa mpango huo umeoza na ni kero kwa raia wote wa Marekani.
Amesema kuwa mpango huo hauwezi kuleta amani hata kama Iran ikikubaliana na kila kitu kama sehemu ya utekelezaji wa mpango huo uliosainiwa mwaka 2015 chini ya utawala wa rais mstaafu wa nchi hiyo Barack Obama.
Trump amesema kuwa watarejesha vikwazo vya kiuchumi vilivyoondolewa dhidi ya Iran kupitia makubaliano hayo ya mwaka 2015.
Aidha, kwa upande wake Rais wa Iran, Hassan Rouhani amekosoa hatua ya Marekani kujitoa na kudai kuwa haiheshimu makubaliano yake, huku akisema imeenda kinyume na mataifa ya Ulaya yaliyofikia makubaliano hayo.
Hata hivyo, Israel na Saudi Arabia kwa pamoja wamepongeza hatua ya rais Trump ya kurudisha vikwazo dhidi ya Iran ambavyo vinatarajia kuanza ndani ya miezi mitatu.
-
Iran yamtahadharisha Trump kuhusu mkataba
-
Burundi yatakiwa kuruhusu matangazo ya Redio
-
Ethiopia na Kenya zaunda mkakati wa kupambana na ugaidi