Serikali ya Israel imepongeza utendaji wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli katika masuala mbalimbali kwa kipindi kifupi cha miezi miwili tangu alipoingia madarakani.

Sifa hizo za Israel kwa Dk. Magufuli zimewasilishwa jana na Balozi wake hapa nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya, Balozi Yahel Vilan alipotembelea Ikulu jijini Dar es Salaam.

Balozi Vilan alimhakikishia rais Magufuli kuwa serikali ya Israel itaendelea kushirikiana na Tanzania hususan katika masuala ya uchumi kwani ushikiriano huu ni muhimu sana.

Naye rais Magufuli alimhakikishia Balozi huyo kuwa serikali yake itaendeleza na kuimarisha uhusiano uliopo kati yao na kwamba atahakikisha ubalozi wa Tanzania nchini Israel unafunguliwa ndani ya kipindi cha muda mfupi.

“Natambua mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na Israel, mahusiano haya ni muhimu sana kwa ustawi wa nchi zetu mbili, nataka mahusiano haya yaimarishwe zaidi,” alisema rais Magufuli.

Walichozungumza Maalim Seif, Lowassa na viongozi wa Ukawa kuhusu Zanzibar
Nacho Monreal Athibitisha Ni Vipi Anavyoipenda Arsenal