Israel imeshambulia maeneo ya Iran ndani ya Syria ambapo shambulio kubwa ni lile la ndege zake za kivita zilizoshambulia mfumo wa ulinzi wa anga wa Syria na kuanguka.

Kufuatia  mashambuliano hayo makali baina ya mahasimu hao wakubwa Israel na Iran tangu vita vya wenyewe kwa  wenyewe nchini Syria kuanza mwaka 2011, waziri mkuu, Benjamin Netanyahu ameapa kuizuia Iran kuweka majeshi  yake katika taifa hilo la Kiarabu.

Aidha, mashambulizi hayo ya Israel yamekuja baada ya ndege ya Iran isiyokuwa na rubani kuingia katika anga la nchi hiyo ikitokea Syria, kitendo ambacho imekiita ni shambulio.

Marekani imeiunga mkono Israel na kuilaumu Iran kwa kuchochea uhasama, huku Katibu mkuu wa Umoja wa  Mataifa, Antonio Guterres akitoa wito wa kuachana na hali ya kuchochea ghasia.

Hata hivyo, Msemaji wa jeshi la Israel, Jonathn Conricus ameonya kuwa Syria  na  Iran zinacheza na moto lakini alisisitiza kwamba  nchi yake haitaki kuendeleza mzozo huo.

 

 

Video: Mkwara wa Makonda nusura uue, Chadema, Cuf walia hujuma Kinondoni
Tanzania yajiondoa Umoja wa Mataifa