Israel imetoa mwaliko kwa wananchi wa Tanzania kutembelea miji yake mitakatifu iliyopo nchini humo ili kuweza kujionea vitu mbalimbali.
Aidha, katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania, Devotha Mdachi imesema kuwa Israel imepunguza kiwango cha gharama za utalii kiasi ambacho watanzania wengi wataweza kukimudu.
“Nawaomba watanzania kutumia fursa hii kwa sababu mbali na masuala ya uhujaji watakutana na wenzao wa Israel ambao nao watataka kuitembelea Tanzania,”amesema Mdachi.
Hata hivyo, balozi wa Tanzania nchini Israel, Job Massima amesema kuwa raia wa Israel wanawapenda watanzania ndio maana wametoa mwaliko huo kwa kupunguza gharama mbalimbali za kutembelea baadhi ya miji mitakatifu ya nchi hiyo.