Jeshi la Israel limewafyatulia makombora watu wanne waliokuwa wanapanda mabomu kwenye uzio wa mpaka wake na Syria.

Wanajeshi wa Israel waliwaona watu hao Jumapili, Agosti 2, 2020 majira ya usiku, na waliamua kuwafyatulia makombora kutoka mbali, kwa mujibu wa taarifa rasmi ya jeshi la Israel.

“Wakiungwa mkono na vikosi vya anga, wanajeshi wetu walirusha makombora kwa pamoja kulenga kundi la magaidi wanne,” imeeleza taarifa hiyo.

Msemaji wa jeshi hilo amesema kuwa ni mapema sana kutaja kundi lolote kuwa linahusika, lakini Israel inaamini Serikali ya Syria inapaswa kuwajibika.

Hata hivyo, Syria haikutoa tamko lolote la kujibu tuhuma hizo kutoka kwa Israel ambao ni hasimu wake.

Taharuki ilizuka zaidi wiki kadhaa zilizopita kati ya Israel na Syria kufuatia mashambulizi yaliyotekelezwa na Israel na kumuua mpiganaji wa kundi la Hezbollah katika kingo za Damascus.

Israel imeongeza nguvu na kufanya mashambulizi kadhaa katika eneo la Kaskazini Mashariki kwenye mpaka wake na Lebanon pamoja na Syria.

Ripoti: Korea Kaskazini yaunda kombora jipya dogo la nyuklia, ‘UN’ yaitahadharisha dunia

Jeshi lamkamata kigogo wa dawa za kulevya aliyemjaribu Rais

15 wapitishwa Tuzo za VPL 2019/20
Ripoti: Korea Kaskazini yaunda kombora jipya dogo la nyuklia, ‘UN’ yaitahadharisha dunia