Klabu ya Azam FC imeendelea kushusha vifaa, baada ya kumtangaza mchezaji wanne wa Kimataifa, ikiwa ni muendelezo wa usajili kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu na Michuano ya Kimataifa msimu wa 2022/23.
Azam FC leo Ijumaa mchana (Julai Mosi) imemtangaza Kiungo kutoka nchini Nigeria Isah Ndala, ambaye aliwahi kuja Tanzania na klabu ya Plateu United iliyocheza na Simba SC katika hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika msimu wa 2019/20.
Ndala alionyesha uwezo mkubwa katika michezo yote dhidi ya Simba SC, na kuibua gumzo kubwa miongoni mwa wadau wa soka la Bongo, huku young Africans wakihusishwa kumsajili kwa msimu uliopita lakini haikuwa hivyo.
Azam FC imethibitisha kumsajili kiungo huyo kupitia kurasa zake za Mitandao ya Kijamii ikiandika: Tumefanikiwa kunasa saini ya kiungo mkabaji kutoka Nigeria, Isah Ndala, tukiingia naye mkataba wa miaka miwili.
Ndala aliyekuwa akichezea Plateau ya Nigeria, amesaini mkataba mbele ya mmiliki wa timu, Yusuf Bakhresa @yusufbakhresa na Afisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin @abdulkarim.amin.
Kiungo huyo, mwenye umbo kubwa, sifa ya ukabaji na kupiga pasi, anakuja kuimarisha eneo la kiungo, ambapo Septemba mwaka huu atakuwa anatimiza umri wa miaka 20.
Aidha mbali na kucheza Plateau, Ndalla amepita pia katika timu ya Sevan ya Armenia na Nasarawa United ya Nigeria.
Huo unakuwa ni usajili wetu wa tatu kuelekea msimu ujao, baada ya jana kuwatangaza nyota wawili kutoka Ivory Coast, Kipre Junior na Tape Edinho.
Welcome to Azam FC kiungo matata, Isah Ndala. ⭐?
#WeAreAzamFC #TimuBoraBidhaaBora