Italia imetishia kupiga marufuku kupokea wahamiaji wote ambao wanaingia nchini humo kinyume cha taratibu za nchi hiyo.
Hayo yamesemwa na mwakilishi wa taifa hilo katika mkutano wa jumuiya ya umoja wa Ulaya, Maurizio Massari, ambapo amesema idadi ya wahamiaji kutoka Afrika ya Kaskazini inazidi kuongezeka.
Aidha, Kamishna wa jumuiya ya Uhamiaji ya Umoja wa Ulaya EU, Dimitris Avramopoulos amesema kuwa kila nchi katika umoja huo inajukumu la kibinadamu la kuweza kuokoa maisha ya binadamu hasa ya wahamiaji hao ambao wengi wao wamekuwa wakikimbia machafuko nchini mwao.
Hata hivyo, Umoja huo wa Ulaya umetenga nusu ya Euro milioni mbili ili kuweza kukabiliana na wimbi hilo la wakimbizi kutoka Afrika.