Mlinda lango wa klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, Itumeleng Khune amepanga kukutana na uongozi wa klabu hiyo baada ya michezo ya kuwania  kufuzu Fainali za Afrika 2021 ‘AFCON’, ili kufahamu hatma yake klabuni hapo.

Mkataba wa Khune na ‘Amakhosi’ unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu, na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 huenda akapewa mkono wa kwaheri ndani ya klabu yake hiyo ya maisha.

Kiungo, Lebogang Manyama ni mchezaji mwingine muhimu ambaye hatma yake huko Chiefs bado haijulikani na klabu bado haijaamua ikiwa watambakiza msimu ujao.

Manyama alikosa mchezo wa  Ligi Kuu ya Afrika Kusini dhidi ya Orlando Pirates ‘Soweto Derby’ uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita, kwa sababu ya kusimamishwa.

Wachezaji wengine wanaohusishwa kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu ni pamoja na Bernard Parker, Willard Katsande na Siphosakhe Ntiya-Ntiya.

Kaizer Chiefs inasemekana inajiandaa kwa dirisha kubwa la uhamisho mwishoni mwa msimu huu na rundo la wachezaji wanaweza kuachwa na zaidi ya wachezaji 10 watakuwa wapya na mazungumzo baadhi yao yameanza kufanyika.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Machi 26, 2021
Mwanahamisi aelezea ufundi wa soka la Morocco