Kiungo Mshambuliaji wa Tottenlham, Ivan Perisic huenda akawa nje ya dimba hadi msimu ujao baada ya kuumia goti kwenye mazoezi ya timu hiyo.

Kutokana na jeraha hilo limewafanya mashabiki kupata hofu kwani mchezaji huyo alionyesha kiwango kizuri tangu msimu ulipoanza.

Spurs ilithibitisha Jumatano kwamba Perisic alipata jeraha hilo akiwa mazoezini na atafanyiwa upasuaji wa goti.

Taarifa ya klabu ilisema: “Tunaweza kuthibitisha kwamba Ivan Perisic amepata majeraha la goti la mguu wa kulia na atafanyiwa upasuaji. Tunamtakia kila la kheri apone haraka,”

Taarifa hiyo pia iliwapa hofu wachezaji wenzake huenda asicheze tena kufuatia jeraha hilo la goti. Perisic alicheza mechi zote tano za ligi kuu ya England akitokea benchi msimu huu.

Mechi ya mwisho kucheza katika Ligi Kuu England ilikuwa dhidi ya Sheffield United wikiendi iliyopita na kuisaidia Spurs kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Nyota huyo wa zamani wa Inter Milan mkataba wake utamalizika mwakani na huenda akaachwa kwenye usajili wa dirisha la kiangazi mwakani kwa mujibu wa ripoti.

Inonga atibua mipango Simba SC
Young Africans yaanza mikakati ya makundi CAF