Ivory Coast imempa hati za kusafiri aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Laurent Gbagbo, na kumruhusu kurudi nyumbani kutoka uhamishoni Ubelgiji, kabla ya mwaka kumalizika. 

Taarifa iliyotolewa na wakili wa Gbagbo, Habiba Toure imeeleza kuwa kiongozi huyo wa zamani ameshapokea hati mbili za usafiri, moja ya kidiplomasia na moja ya kiraia akiwa mjini Brussels na atarudi Ivory Coast kabla ya mwaka kumalizika. 

Hatua hiyo ya Ivory Coast inafuatia kiongozi huyo wa zamani kufutiwa mashtaka katika kesi ya uhalifu wa kivita iliyokuwa inamkabili katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, ICC. 

Mahakama ya ICC yamuombea hifadhi Gbagbo Ubelgiji

Gbagbo amepokea hatua hiyo kama ishara ya maridhiano kutoka kwa Rais Alassane Outtara, ambaye mvutano mkali kati yakena wapinzani kuhusu kuchaguliwa kwake kwa muhula wa tatu, umezusha maswali juu ya uthabiti wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi, uliopatikana kwa kazi ngumu.

Mwaka 2018 Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC ilimuombea Gbagbo hifadhi nchini Ubelgiji, mara baada ya kuachiwa huru na mahakama hiyo.

Serikali kununua ndege zingine 4
Mapigano yakwamisha misaada Tigray