Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema kuwa kamwe serikali ya Tanzania, haitaruhusu ushoga na kwamba kila kiungo kilichoumbwa na Mungu kwenye mwili wa mwanadamu kina kazi yake.
 
Ameyasema hayo mara baada ya Mbunge wa Jimbo la Konde (CUF), Khatibu Saidi Haji, kusema anashangazwa na serikali kuwa na kauli laini kuhusu vitendo vya ushoga lengo likiwa ni kubembeleza
 
“Msiseme kuwa labda serikali inajichanganya kwenye jambo hili, ni maelekezo ambayo tunatoa labda vyombo vinaripoti tofauti, lakini serikali yetu kamwe, Tanzania ni hekalu la roho mtakatifu. hatuwezi kukubali hekalu la roho mtakatifu likatumika kwa mambo ambayo hayakubaliki,” amesema Lugola.
 
Aidha, katika mkutano wake na waandishi wa habari Oktoba 31, 2018, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda alitangaza kampeni ya kukabiliana na vitendo vya ushoga katika jiji la Dar es salaam, ambapo aliunda kamati ya watu 15 kwa ajili ya kupambana na wanaojihusisha na ushoga, wanaotapeli wengine kwa kutumia mitandao wakijifanya ni viongozi maarufu nchini.
 
Baadaye Novemba 4, Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ilitoa msimamo wake juu ya sakata la Mkuu wa Mkoa wa Dar es saalam dhidi ya ushoga katika mkoa wake nakudai kuwa ni mawazo yake na si msimamo wa serikali.
 
  • Raia wawili wa Kichina watupwa jela
  • Wanunuzi wa Korosho sasa kufutiwa leseni, wapewa siku nne
  • GGM yalalamika watoto kuvamia mgodini
Hata hivyo, Novemba 7, katika mkutano wake na vyombo vya habari, Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Kangi Lugola aliwahakikishia usalama watu wanaojihusisha na mapenzi jinsia moja nchini (Mashoga) na kwamba hakuna atakayewakamata

NEC yatoboa siri ya wabunge waliohama Chadema kupita bila kupingwa
Video: Biashara konki zenye pesa ndefu na hufanywa na watu wachache zaidi duniani