Hatiame kiungo wa klabu ya Aston Villa,  Jack Grealish amefanya maamuzi ya kuchagua kuitumikia timu ya taifa ya England, baada ya kujifikiria kwa kina na kuona umuhimu wa kujikita katika utaifa wa nchi hiyo.

Grealish,  alikua katika hali ya sintofahamu ya kuchagua ni wapi anapostahili kucheza kwa upande wa timu ya taifa, kutokana na mzozo ulioibuka baina ya mataifa ya England dhidi ya Ireland ya kaskazini ambayo yalikuwa yakitoa ushawishi dhidi yake ili akubali kujiunga na moja ya pande hizo mbili.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20, alipata nafasi ya kuzungumza na makocha wa timu za mataifa hayo Roy Hodgson pamoja na Martin O’Neill ili kujua mustakabali wake kwa maamuzi ambayo alitarajiwa kuyachukua.

Grealish, alizaliwa nchini England katika kitongoji Solihull, ambapo wazazi wake ndipo wanapoishi mpaka sasa, lakini ana asili ya Ireland ya kaskazini.

Hata hivyo Grealish, aliwahi kuitumikia timu ya taifa ya vijana ya Ireland ya kaskazini, lakini kanuni na taratibu za FIFA hazikumfunga katika kufanya maamuzi ya kuchagua ni wapi atakapocheza akiwa na umri wa mtu mzima.

Maamuzi yaliyochukuliwa na Grealish, huenda yakawa na bahati ya kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England, ambacho kitatajwa mwishoni mwa juma hili na kocha Roy Hodgson, kwa ajili ya michezo ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya barani Ulaya za mwaka 2016 dhidi ya Estonia pamoja na Lithuania.

Mtoto Wa Paul Walker Afungua Mashtaka Kuhusu Gari Lililochukua Uhai Wa Baba Yake
Lukaku Atuma Salamu Anfield